May 16, 2013

Apple App Store imefikia downloads za application zipatazo bilioni 50

Apple wamefikia kiasi cha applications bilioni 50 ambazo zimedownloadiwa na watumiaji wa iPhone na iPad.Stoo hii ilifunguliwa rasmi mwaka 2008 na baada ya hapo imekua kwa kiasi kikubwa na kuwa moja ya stoo maarufu sana duniani.

 Hiyo ni picha yao iliyoonekana katika mitandao mbalimbali ya internet ikishukuru kwa watu wote waliofikisha kiasi kama hicho.Apple wameweka kijisehemu ambapo kinaonesha ni kiasi gani application zinavyokuwa downloaded na mtu atakaye download application na kufanya namba hiyo kufikia bilioni 50 anapewa kadi ya dola 10000 za kimarekani itayomwezesha kununua applications katika App Store.Wameweka pia bahati nasibu ambapo mshindi katika droo atazawadiwa kadi ya dola 500.Washindi bado hawajatangazwa,ila hivi karibuni wote watatangazwa na kupewa zawadi zao.

No comments :

Post a Comment