May 18, 2013

Aina za vioo vinavyotumika katika smartphone ili kuzuia michubuko na mipasuko.

Makala hii itakueletea maelezo kuhusu aina za vioo vinavyotumika katika simu mbalimbali ili kuzuia kuharibika kwa kioo cha simu aitha kwa kuchubuka au kwa kuvunjika,vioo hivi si kwamba havivunjiki kabisa au kuchubuka ila vinazuia kwa kiasi kikubwa ile michubuko na mivunjiko ya kawaida ambapo kioo cha kawaida kisingeweza kuhimili.

Kuna makampuni mengi yamefanikisha kutengeneza aina ya vioo hivi ambapo ilichukua muda sana katika kupata aina hii ya kioo.Kampuni ambazo ni maarufu kwa sasa kwa kuzalisha hivi vioo ni Corning Co. ambao kioo chao kinaitwa Gorilla Glass,Asahi Glass Company(AGC) ambao kioo chao kinaitwa Dragontrail na Schott AG kioo chao kinaitwa Xensation.Nitaongelea hivi vioo vitatu hasa katika makala hii.


GORILLA GLASS

  Hiki ndicho kioo kinachotumika sana katika simu,tablet na hata televisheni.Kina uwezo mkubwa wa kuhimili mgandamizo au kitu chenye ncha kali kama kisu kinaposugua juu yake na kina kipimo kwa kitaalamu kinaitwa Vickers hardness test kuanzia 622 hadi 701.Kilizinduliwa rasmi mwaka 2007 ambapo kwa mara ya kwanza kiliwekwa katika simu ya Apple iPhone.Baada ya hapo simu nyingi zilianza kutumia hiki kioo.Mpaka mwaka 2010 kilikuwa kinatumika kwa asilimia ishirini katika simu dunia nzima.Gorilla Glass 2 kizazi cha pili cha hii bidhaa kilizinduliwa mwaka 2012 hadi kufikia tarehe 24 mwezi wa kumi,Corning walitangaza devices zinazotumia zimefikia zaidi ya bilioni moja.Gorilla Glass 3 kizazi cha tatu cha hii kilizinduliwa january 7 mwaka huu,na kikiwa na maboresho makubwa sana ukifananisha vioo vya nyuma kama gorilla 1 na 2.Kioo hiki kimetumika katika simu za iPhone,Samsung Galaxy s4 na nyingine nyingi ambazo zimetoka hivi karibuni zilizo za hali ya juu(high end devices). http://m.corninggorillaglass.com/smartphone,hiyo ni link ya kukuonesha listi ya device zinazotumia hiki kioo.

DRAGON TAIL

 Hiki ni kioo kinachozalishwa na kampuni ya Asahi Glass Company,ni chembamba,chenye wepesi na kinachoziuia kuharibika kina kipimo cha Vickers hardness test kuanzia 595 hadi 673.Kilizinduliwa mwaka 2011 na kinatumika na simu nyingi za Sony Xperia kama Xperia Z,Xperia active,MI2 simu ya kampuni ya kichina iitwayo Xiaomi na Galaxy Nexus.



  Bidhaa hizi mbili zimekuwa na ushindani katika soko na hupendwa kulinganisha katika mitandao mbalimbali ili kuonesha kipi ni bora zaidi.

 XENSATION

 Hiki ni kioo kioo kinachotenezwa na kampuni ya Schott AG,matumizi ni kama yalivyo ya vioo vingine vilivyopita hapo juu na pia hiki bado hakijapata umaarufu sana katika kutumika katika simu na tablet.Mwaka jana walikizndua hiki kioo na kusema ni kinaweza kupinda kwa asilimia 20 zaidi ya Gorilla Glass na Dragontrail.

Vioo hivi ni muhimu sana katika kulinda devices zetu,simu kuwa na kioo kati ya hivi vitatu haimaanishi kwamba kioo hakitavunjika au kutochubuka bali kitaweza kuhimili ile misuguo ya kawaida tu.Punguza hatari ya kupata michubuko au mipasuko kwa kuweka simu yako na vitu vya chuma katika mfuko mmoja mfano funguo au sarafu na pia kuepuka kudondosha simu mara kwa mara,kwa hivi utaweza kuwa na simu kwa muda mrefu sana bila michubuko wala kupasuka.


No comments :

Post a Comment