May 26, 2013

Mvumbuzi wa simu za BlackBerry amesema watumiaji wa iPhone wataipenda sana BBM inayokuja hivi karibuni katika simu zao.


Mmiliki wa kampuni ya RIM inayotengeneza simu za BlackBerry amesema ana uhakika kabisa kwamba application ya BBM itapokuja katika simu za iPhone itapendwa sana na watumiaji wa simu hizo.Hivi karibuni RIM walitangaza kuwa BBM itapatikana katika simu za Android na iOS(cross platform) miezi michache ijayo. Alisema hayo katika mkutano wa kiuchumi uliofanyika huko Canada,kampuni hii iko Waterloo,Ontario huko nchini Canada.Mpaka sasa BBM inatumiwa na wateja wapatao milioni 60 dunia nzima ambao kwa makadirio hutuma sms bilioni 10 kwa siku.Haijaeleweka mpaka sasa ni vipi kampuni hii itafaidika na uamuzi huu wa kupeleka BBM kaika Android na iOS.

 Toka kujitoa kama mkurugenzi mtendaji wa RIM na kumuachia Thorstein Heins amekuwa akishughulika na teknolojia ya quantum-computing  na nanotechnology.Hii ni teknolojia inahusika zaidi na vitu vinavyokaribia kwa ukubwa na atomu.Baada ya miaka michache tekonolojia hii itakuwa ndo inatumika kuunda vifaa vingi vya kielectroniki na ambapo itawezekana kuwa na hata na smartphone wembamba kama wa karatasi.







No comments :

Post a Comment