May 23, 2013

Je?smartphones zitaweza kubadili Afrika katika mtazamo wa kiteknolojia?

Hivi Karibuni kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika upande wa teknolojia,nakumbuka zamani nilipokuwa mdogo ilikuwa ni nadra sana kuona mtu ana simu ya mkononi na hata wale waliokuwa nazo walikuwa ni watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha.Lakini sasa hali ni tofauti ambapo hadi watoto wa shule za vidudu(kindeegarten) wanamiliki simu na tena usishangae kuona ni smartphone.Lakini swali linakuja,Je!mabadiliko haya yataweza kuibadili Afrika katika uono wa kiteknolojia? Tumeona mabadiliko makubwa katika nyanja ya sayansi na teknolojia kidunia hasa kuanzia mwaka 2007 ambapo simu za Android zilianza kutoka na Htc ikiwa ni kampuni ya kwanza kutumia Operating System hii.Lakini kwa Afrika mabadiliko makubwa yamekuja mwaka 2009 na kwa Tanzania yameonekana katika mwaka 2011.Sasa hivi karibu vijana wengi na watu wazima wanatumia smartphones haijalishi ni low end,mid range au high end ari mradi ni smartphone. Makampuni kama Microsoft na Huawei yameungana kwa makusudi ili kutengeneza simu kwa ajili ya Afrika ambazo ni smartphones ila za bei nafuu,si kusema kwamba hazina ubora,la hasha!Simu hizi zinatengenezwa kwa kuangalia mahitaji ya Kiafrika na pia kuiwekea mazingira(customization) ya urahisi kutumia.Kuna simu ilizinduliwa mwezi wa pili mwaka huu na kampuni ya Huawei ikiwa inaitwa Huawei 4Afrika ambayo inatumia operating system ya Windows Phone 8 ambayo inatengenezwa na kampuni ya Huawei.Ujio wa simu hii si faida tu kwa watumiaji bali inafungua dunia ya uwezekano kwa watengenezaji wa softwares wa Afrika ambapo wateweza kutengeneza softwares ambazo zimekaa katika mazingira ya kiAfrika na watu wa Afrika kutumia simu hizi kwa urahisi.




Toka kuzinduliwa kwa simu hii kuna ongezeko kubwa sana la wanafunzi na wafanyakazi katika kutumia simu katika shughuli zao za kila siku  barani Afrika,lakini kwa nchi kama Tanzania namba hii bado ni ndogo sana kwa sababu kuna uelewa mdogo wa watu katika kujua nini kazi hasa ya smartphone.Wengi wa watu hudhani ni simu kwa madhumuni ya kusikiliza muziki katika raha na kuangalia movies na kucheza games.Hili sio dhumuni kuu la smartphones na wengi wao huweka pembeni dhumuni kuu,ni wachache sana wanaotumia katika kufanya kazi zao za darasani kwa kutumia smartphones zao na hata watu wa ofisini pia.Jambo hili linatakiwa kubadilika muinekano wake na tuwe kweli wa kufaidika na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Ni muhimu sana kwa smartphones kutumika kama kifaa cha kujifunzia na sio kifaa cha burudani kama wengi wanavyochukulia.Katika nchi kama Afrika ya Kusini makampuni mengi sasa yanatengeneza softwares ambazo wafanyakazi wao watakuwa nazo katika simu zao zitazowawezesha kufanya kazi za ofisi popote waendapo na pia kupata mafunzo(training katika kupitia simu za video).Je?unatumia simu yako kwa usahihi?ni mimi,wewe na yule ndio tutaleta mabadiliko ya uelewa wa teknolojia Afrika.

No comments :

Post a Comment