May 16, 2013

Mpambano kati ya BBM,Whatsapp na Viber,tuone utofauti wao na ipi inapiku wenzie.

BlackBerry mapema wiki hii imetangaza kwamba italeta application yake ya kijamii ya BBM katika simu za android na iphone.Huo utakuwa ni mchuano mkubwa sana na apps hizi kuu nyingine kama Whatsapp na Viber ambazo ni cross platform(application zinazopatikana katika operating system zaidi ya moja).

iMessage inakuwezesha pia kutuma sms na picha kwa kutumia internet lakini inapatikana katika simu za Iphone tu kwa hiyo huyu hausiki katika mchuano huu.

BBM



Gharama ni bure na itapatikana pia bure katika Android na iOS. Inatoa huduma ya kutuma sms,picha,video na muziki lakini kwa BlackBerry10 OS unaweza ongea na mtu(Voip),yaani voice through internet protocol na pia unaweza kuongea nae kwa kuonana yaani video chat.Ili kupata mtu wa kuchat nae lazima umualike kwa kutumia pin yake hii ni namba maalumu inayokuwa na simu ikiwa na mchanganyiko wa namba na herufi jumla yake yake nane mfano.23714CGF,lakini hata hivyo BlackBerry hawajasema kwamba BBM itapokuja kwa Android na iOS itaendelea kutumia mfumo huu wa sasa wa pin kitu ambacho kitamuangusha ukiangalia kwamba hawa wenzake wanatumia namba za simu kwa hiyo huitaji kushughulika sana kutafuta watu wa kuchat nao unapotumia whatsapp au viber.

VIBER






Gharama ya viber ni bure pia na huwa hawatengenezi hela yoyote katika app yao kwa sababu hawajaweka matangazo yoyote unapotumia viber.Inapatikana katika smartphones mbalimbali kama iPhone,Windows Phone,Android,BlackBerry lakini bado haijatoka kwa simu za BlackBerry 10,Windows desktop,Mac Os X na hata Symbian na Bada.Kwa iPad bado haijatoka lakini iko njiani kuja katika tablet hiyo. Pamoja na kwamba unaisajili katika simu moja kwa kutumia namba yako ya simu lakini unaweza kweda kutumia katika device nyingine yoyote na kuona zile sms zote ulizpchat katika simu nyingine.Iko simple ukilinganisha na wenzake na pia huwa inakujulisha pale mmoja wa namba zako anapoanza kutumia hii application,hauwezi piga simu za video kwa sasa katika simu lakini uwezo huu unapatikana katika kompyuta.


WHATSAPP

 Gharama yake ni bure katika kudownload kwa simu za android,blackberry na windows phone na mwaka mmoja bure kutu,ila baada ya hapo utatakiwa kulipia dola za kimarekani 0.99 kwa mwaka lakini kwa iPhone unatakiwa kuinunua wakati unapotaka kutumia,kama unataka kuidownload kwa free lazima hiyo iPhone iwe jailbroken.         






 Ni rahisi kuitumia,inapatikana katika android,windows phone,blackberry,symbian na iOS .Ni rahisi kupata watu wa kuchat nao kwa sababu inatafuta yenyewe watumiaji wa whatsapp katika simu yako na watatokea katika list iitwayo favourite.










Whatsapp imekaa zaidi kama application ya simu kabisa kwa ajili ya kutuma sms tofauti na wenzake.




HITIMISHO

 Huduma zote hizi tatu zinafanya kazi sawa ya kutuma sms,video,picha na kadhalika.Lakini Viber ndo inapatikana katika operating system nyingi kuliko wengine.Lakini imeonekana na matatizo ya software katika simu nyingi na pia ikihitaji maboresho.


 Bila kujua kwa uhakika kwamba BBM katika Android na iOS itakuwa na muonekano gani,haijafahamika kama ataweza kuwashinda wenzake.Kama ataleta muonekano uliopo katika BlackBerry 10 kama kupiga simu za video,kushare screen na kupiga simu za sauti basi ataleta mchuano mkubwa sana na kuweza kuzishinda viber na whatsapp.





















  


1 comment :

  1. Very great post. I just stumbled upon your blog and wished to say that I've truly enjoyed surfing around your weblog posts. In any case I will be subscribing in your rss feed and I'm hoping you write again soon!


    my blog post :: whatsapp for samsung phones

    ReplyDelete