May 15, 2013

Kampuni ya Google yatangaza kuwa na simu zipatazo milioni mia tisa mpaka sasa zinazotumiika ambazo zinatumia Android OS.

Mkutano wa Google I/O umeanza na Google ambayo ndo kampuni inayomiliki Android operating system imetangaza mpaka sasa imeuza simu zipatazo milioni mia tisa ambazo zinatumika. Ukuaji huu unaonesha haujakwama hata kidogo,Sundar Pichai ambaye ndo anashikilia nafasi ya head of project ya Android,Chrome na Apps ametangaza hii namba leo katika mkutano huo unaoendelea.Sundar Pichai amesema pia bado kuna ukuaji mkubwa ambao unategemewa.Asia na Africa zimeripotiwa kuwa na mchango wa asilimia 10 tu na amesema pia wanafanya kazi kuwa na watu bilioni nne na nusu kwenye internet wanaotumia Android,mbali na hilo wametangaza installation bilioni arobaini na nane katika Google Play Store.

No comments :

Post a Comment