May 23, 2013

LG vs Samsung,hadithi iliyonyuma kuhusu mapambano kati ya hizi kampuni mbili kubwa za kutengeneza vifaa vya kielectroniki.

Ushindani kati ya LG na Samsung unafahamika wazi.Kampuni hizi mbili ambazo ni za Korea ya Kusini ambazo makao makuu yao yapo Seoul yamekuwa katika ushindani kwa zaidi ya miaka 50.Kila mmoja huwa anaangalia mwenzake atafanya nini kipya ili na yeye aje na zaidi ya kile anacvhotaka kuzindua mwenzie.Siri zimeibiwa,tuhuma zilishatokea,mahakamani kesi zishapelekwa kwa kugombea umiliki halali wa baadhi ya uvumbuzi kati ya haya makampuni mawili kila mmoja akitafguta udhaifu wa mwenzie.Wiki chache zilizopita kulikuwa na mashtaka kuhusu nani ambaye ndo ameanzia teknolojia ya OLED(Organic Light Emitting Diode). Hivi karibuni polisi walivamia moja ya ofisi za Samsung ili kuchunguza baada ya LG kudai anafatiliwa uvumbuzi wake na Samsung.Na hata inafikia kiasi kwamba ulinzi uliopo katika makao makuu ya ofisi hii ni mkali zaidi ya ule wa uwanja wa ndege.Mabegi hukaguliwa,kamera zinaachwa nje,kifaa chochote chenye kuhifadhi kumbukumbu(USB Storage) hakiruhusiwi na kamera za usalama zipo kila kona. Haishangazi kwamba kampuni zote hizi mbili zinaongoza kwa kutengeneza vioo(display) zenye ubora wa hali ya juu.Lakini,huwa mara nyingi wanaleta bidhaa zimazofanana,mfano;mwaka huu wote walileta TV ya kwanza ya teknolojia ya OLED yenye mikunjo(curves). Mbali na hayo yote kampuni hizi sio teknolojia tu,ni mfumo wa maisha na watu wengi sana waliojiriwa katika makampuni haya wako radhi kutumia muda wote kufanya kazi katika makampuni haya mpaka muda wa kustaafu utapowafikia.Tofauti na makampuni makubwa ya Ulaya na Marekani haya yanajitoa sana katika kukuza uchumi wa nchi yao,kila mwaka huchukua vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali na kuwaajiri na wengi wao huwa wanaishia kufanya kazi katika makampuni haya mpaka wanapokuja kustaafu.

No comments :

Post a Comment