May 20, 2013

LG kuzindua simu ambayo unaweza kuikunja na bila kuvunjika(flexible smartphone)

Kampuni ya Korea ya kusini ya vifaa vya kielectroniki ya LG iliwahi kutangaza miezi ya hivi karibuni kwamba itazindua aina ya simu ambayo utaweza kuikunja bila kuvunjika.

 Simu inategemewa kuzinduliwa katika maonesho yaitwayo Display Week 2013.Hili ni tukio ambalo huonesha bidhaa zinazotumia vioo vya kielectroniki na litafanyika wiki huko Vancouver,Canada.

 Aina ya teknolojia inayotumika katika vioo vya simu za LG inaitwa Organic Light Emitting Diode(OLED) ambayo huokoa nishati kwa kuhitaji matumizi madogo ya chaji katika betri ili kufanya kazi,ni chepesi na ndo maaana simu nyingi za LG ni nyepesi na pia ni chembamba ukifananisha na simu zinazotumia teknolojia ya LCD(Liquid Crystal Display).

 Kwa kunukuu wamesema"Simu hii inakuja katika wakati ambao smart devices zinatumika sana na haijwahi pata tokea na hatari za simu kudondoka na kuvunjika zikiwa kubwa sana"


 Bwana  Yoon Bu-hyun makamu raisi wa kampuni hiyo alitangaza wazi mwezi jana kwamba simu hii itazinduliwa katika robo ya mwisho ya mwaka.


 Hata hivyo makampuni mengine yanaitolea jicho hiyo teknolojia .Katika mkutano wa Computer Electronics Show uliofanyika mapema mwaka huu Samsung alionesha teknolojia kama hii na kuiita Youm,ambayo itawezesha kutengeneza vioo ambavyo vinakunjika,kuviringisha na hata kupinda.












































No comments :

Post a Comment