May 21, 2013

Itsdagram sasa inapatikana katika simu zinazotumia Windows Phone 8 ikiwa na muonekano kamili kama wa Instagram.

Wiki chache zilizopita tulitoa taarifa katika blog yetu kwamba Instagram inakuja katika simu za Windows Phone.Habari hii sasa imetimia.



Itsdagram sasa inapatikana katika windows phone 8.Ila hii sio application rasmi lakini itatumika mpaka application rasmi itapokuja.Tofauti na Instagraph,hii application inaruhusu kufanya vyote vile ambavyo unaweza fanya katika Instagram kama inayopatikana katika Android au iOS.Katika simu zinazotumia Windows Phone 7 itakuja baadaye,Kwa sasa inapatikana katika marketplace kwa dola za kimarekani 1.49,hii ndo hasara mojawapo ya windows phone application nyingi nzuri inakuta zinauzwa,tofauti na Android.

No comments :

Post a Comment