May 14, 2013

BB wametangaza simu mpya ya BlackBerry Q5 inayotumia BB10 ambayo ni bei nafuu

Mwanzo wa mkutano wa mwaka wa BlackBerry uliofanyika Orlando,Florida,USA umezindua mambo mengi ikiwamo kutangaza updates ya software kwa simu za blackberry 10 kama z10 na q10,kutambulisha kwamba BBM inakuja katika simu zinazotumia operating system za android na iOS. Pamoja na hayo yote wamezindua simu mpya iitwayo blackberry q5 inayotumia operating system ya BlackBerry 10.Simu hii ina touchscreen ya inchi 3.1 na pia qwerty keyboards,kioo chake ni aina ya LCD chenye resolution ya 720x720px kama ilivyo kwa simu yao ya hali ya juu ya blackberry q10.Ina processor yenye dual core,maana yake ina CPU mbili na internal memory ya 8GB pia kuna slot ya kuwekea memory card lakini battery yake sio ya kutoa nje. Simu hii itapatikana Ulaya,Mashariki ya kati,Africa,Asia na Latin America,itakuja na rangi nyeusi,nyeuoe,nyekundu na pink. Kwa sasa skype haipatikani katika simu mpya za BlackBerry kama q10 na z10 ila wametoa update ambayo ni bb10.1 ambapo sasa wataweza kudownload Skype.

No comments :

Post a Comment