Si tu uwe katika sehemu isiyo na nishati ya umeme ndipo ushindwe recharge simu yako, kuna wakati umeme hukatika, na suala hili ni kawaida. Ina maana kwamba utakwama katika shughuli uliyokuwa ukifanya. Ni afadhali ukiwa unasikiliza muziki, utaburudika tena baadaye lakini isiwe ni wakati ambao ulikuwa ukisubiri simu muhimu sana na hauna mbadala wa kupata tena mawasiliano. Lakini, pengine ungekuwa simu yenye uwezo wa kubadili battery(removable battery) ungeweza kuepuka zahama hii.
Showing posts with label smartphone. Show all posts

Mar 9, 2015
Umuhimu wa smartphone yenye battery inayoweza kutolewa(removable battery).
Watu wengi wanatumia smartphones kwa shughuli mbalimbali, iwe ni kuperuzi mtandaoni, kusikiliza muziki, kupiga picha, kutuma barua pepe au kuchati. Yote haya hutumia nishati kubwa sana ya umeme katika smartphones. Simu hizi hazina uwezo mkubwa wa kuhimili kukaa muda mrefu ikiwa na nishati huku ukiitumia mfululizo. Hii inapelekea uhitaji wa kuipa nishati(recharge) smartphone yako mara kwa mara. Ukiwa ofisini, nyumbani au popote pale palipo na umeme suala la kuchaji simu ni rahisi tu. Lakini inakuwaje upo porini, au sehemu yoyote iliyo haina umeme kabisa na hauna nishati yoyote mbadala?
Sep 13, 2014
Baadhi ya mambo unayoweza fanya ili kuepuka kununua smartphone feki.
Watu wengi hujikuta katika wakati mgumu pale wanapohitaji kununua smartphone, haijalishi ni kwa mara ya kwanza au wanapotaka upgrade kutoka smartphone moja kwenda nyingine. Hali hii huja kutokana na kuwa na maswali mengi akilini, Operating System gani inayofaa?, smartphone ipi ina camera bora?, ipi yenye battery inayodumu muda mrefu baada ya kuchaji mara moja tu?, brand ipi ina reputation nzuri katika soko?, hayo ni mambo machache tu, yapo mengi sana. Lakini kuna jambo moja ambalo wengi wetu tulio wanunuzi wa simu hutakiwa kujiuliza, na pengine kushindwa kuzingatia swali hili inaweza leta huzuni na masikitiko makubwa katika manunuzi yetu. "Je! smartphone ninayotaka kununua ni original?". Nitaeleza njia baadhi unazoweza kutumia ili mwisho wa siku katika manunuzi yako jibu la hili liwe "NDIYO" .
Written by
Unknown
Location:Dar-Es-Salaam,Tanzania
Dar es Salaam, Tanzania
No comments
:
Labels:
clues
,
smartphone
Dec 22, 2013
Mwaka 2013 unaishia,tutegemee nini mwakani katika teknolojia ya smartphone?
Mwaka 2013 ni mwaka ambao karibia makampuni yote ya kutengeneza smartphone yalikuwa bize.Mengine katika ubize wa kuhakikisha wanazidi kuwa juu kila siku na kuvuta watumiaji wengi,mfano Apple na Google(Android),wengine wakiwa bize kuhaha kampuni zao zisije kufa,mfano BlackBerry.
Tumeona hatua kubwa sana iliyopigwa katika teknolojia hii ya smartphone.Kila mtu kajitahidi kuonesha kwamba teknolojia inakua kwelikweli na pia yeye ndo mwenye uvumbuzi bora kuliko wenzake katika ushindani.
Kampuni kama Apple na Android wenyewe hawana matatizo makubwa kama ilivyo kwa BlackBerry au Microsoft.Maana yake wana muda mwingi wa kuwaza mambo mazuri kabisa ya kuwaletea watumaiji wa bidhaa zao.
BlackBerry atatumia mwaka ujao kupona kutoka katika maumivu makubwa aliyopata mwaka huu,kwa hiyo kwa chochote atachofanya kitakuwa ni kama utangulizi.Atachofanya ni kupita katika njia zilezile alizopita Google mpaka leo na kupata mafanikio makubwa kiasi hiki katika Android,kwa hiyo sidhani kama atakuja na kitu kikubwa cha kutisha.
Windows kwa sasa anaonesha kukua kwa kasi kidogo,si mbaya.Kuna nchi huko Ulaya ambapo simu zake ni maarufu kuliko iPhone mfano baadhi ya sehemu nchini Italy.Nokia anazidi kutoa simu za Nokia Lumia ambazo zina ubora sana,tabs za Microsoft Surface na pia tabs za Nokia,ingawa bado ndo zinatafuta umaarufu.Labda mwakani atakuja na kitu kipya katika OS yake ya Windows Phone.
Kuna kampuni chipukizi nazo ambazo zinaonekana zikiwa na kasi nzuri,mfano Jolla wanaotengeneza simu za Jolla zinazotumia OS ya Sailfish,Mozilla Firefox nao wana OS yao inaitwa Firefox OS.
Kutakuwa na teknolojia nyingi sana za kusisimua mwakani,usishangae kuona simu ambayo ni kama kioo(transparent) lakini inafanya kazi zote za smartphone pamoja huoni battery wala sakiti.

- Apple kuleta smartphone ya iPhone 5S yenye processor ya 64bit.
- Samsung na LG watengeneza simu ambazo kioo chake kimejikunja(curved display)
- LG waleta teknolojia ya self-healing ambapo simu ya LG G Flex ikichubuka,ule mchubuko unapona ndani ya sekunde chache na panakuwa kama hapajachubuliwa.
- Simu nyingi ambazo zinazuia maji kuingia ndani zimezinduliwa mwaka huu,mfano Samsung Galaxy S4 Active,Sony Xperia Z.
- Camera za smartphone zina pixels kubwa sana kiasi kwamba mahitaji ya digital camera yanapungua,unahitaji simu tu kupiga yenye ubora kabisa.
- Makampuni kama Sony,Samsung wameleta saa ambazo ni smart,zinatumika kama zilivyo smartphone ila yenyewe ni saa na unaivaa mkononi.Unaweza access chochote kilichopo katika simu yako kupitia saa hiyo.Samsung wanaziita Smartgear.
Kampuni kama Apple na Android wenyewe hawana matatizo makubwa kama ilivyo kwa BlackBerry au Microsoft.Maana yake wana muda mwingi wa kuwaza mambo mazuri kabisa ya kuwaletea watumaiji wa bidhaa zao.
BlackBerry atatumia mwaka ujao kupona kutoka katika maumivu makubwa aliyopata mwaka huu,kwa hiyo kwa chochote atachofanya kitakuwa ni kama utangulizi.Atachofanya ni kupita katika njia zilezile alizopita Google mpaka leo na kupata mafanikio makubwa kiasi hiki katika Android,kwa hiyo sidhani kama atakuja na kitu kikubwa cha kutisha.
Windows kwa sasa anaonesha kukua kwa kasi kidogo,si mbaya.Kuna nchi huko Ulaya ambapo simu zake ni maarufu kuliko iPhone mfano baadhi ya sehemu nchini Italy.Nokia anazidi kutoa simu za Nokia Lumia ambazo zina ubora sana,tabs za Microsoft Surface na pia tabs za Nokia,ingawa bado ndo zinatafuta umaarufu.Labda mwakani atakuja na kitu kipya katika OS yake ya Windows Phone.
Kuna kampuni chipukizi nazo ambazo zinaonekana zikiwa na kasi nzuri,mfano Jolla wanaotengeneza simu za Jolla zinazotumia OS ya Sailfish,Mozilla Firefox nao wana OS yao inaitwa Firefox OS.
Kutakuwa na teknolojia nyingi sana za kusisimua mwakani,usishangae kuona simu ambayo ni kama kioo(transparent) lakini inafanya kazi zote za smartphone pamoja huoni battery wala sakiti.
Dec 18, 2013
Je,watengeneza smartphone wanayajua mahitaji hasa ya watumiaji wa smartphone hizo?
Teknolojia ya siku hizi katika mapinduzi haya ya kidigitali tuliyonayo,si ajabu kuja kuona simu ambayo utaweza kuvingirisha kama bangili mkononi pale ambapo umemaliza kuitumia badala ya kuiweka mfukoni.
Tunaona makampuni kama Samsung,Sony na mengineyo wanakuja na bidhaa waziitazo Smartgear.Hizi ni saa za mkononi ambapo utaivaa na kuweza kuaccess chochote kile kilichopo katika simu yako.Inaunganishwa na simu yako kwa kupitia nija ya Bluetooth au Wi-Fi.Ina display kama ile inayotumika katika smartphone.Pia,kuna teknolojia nyingine kama ya display iliyojikunja(curved display) ambayo ipo katika simu kama LG G Flex.
Swali linakuja,tunazihitaji sana hizi teknolojia na nyinginezo za mfumo huu?Kimsingi,hatuzitumii hata kama zikiwepo katika simu zetu.Sidhani kama ni teknolojia zenye manufaa katika kufanikisha kwamba mwisho wa siku tunakamilisha shughuli zetu zinazohusisha smartphones.
Watumiaji wengi wanataka betri yenye nguvu katika simu zao ambayo itakaa kwa siku badala ya masaa.Tatizo ni kwamba,teknolojia ya display imepiga hatua sana na hata ya processor lakini teknolojia ya betri ni ileile tangu miaka ya 2000.Wanachofanya ni kutengeneza betri kubwa ambayo nayo itakaa kwa siku moja na pia inaongeza umbo la simu,mfumo wa teknolojia ya betri unaotumika sasa uko hivi"kadiri betri inapokuwa kubwa na ndivyo uwezo wa kutunza chaji muda mrefu na unakuwa mkubwa"
Kinachohitajika kuonekana katika teknolojia ya simu ni mapinduzi ya hardware katika upande wa betri.Kama watengenezaji watakuja na mawazo mapya na yakafanikiwa katika kubadili ubora wa betri za smartphones,basi hii itakuwa ni furaha kwa kila mtu.Nina imani kubwa hichi ndicho kiu kikubwa cha watumiaji wote wa smartphones.

May 20, 2013
LG kuzindua simu ambayo unaweza kuikunja na bila kuvunjika(flexible smartphone)
Kampuni ya Korea ya kusini ya vifaa vya kielectroniki ya LG iliwahi kutangaza miezi ya hivi karibuni kwamba itazindua aina ya simu ambayo utaweza kuikunja bila kuvunjika.
Simu inategemewa kuzinduliwa katika maonesho yaitwayo Display Week 2013.Hili ni tukio ambalo huonesha bidhaa zinazotumia vioo vya kielectroniki na litafanyika wiki huko Vancouver,Canada.
Aina ya teknolojia inayotumika katika vioo vya simu za LG inaitwa Organic Light Emitting Diode(OLED) ambayo huokoa nishati kwa kuhitaji matumizi madogo ya chaji katika betri ili kufanya kazi,ni chepesi na ndo maaana simu nyingi za LG ni nyepesi na pia ni chembamba ukifananisha na simu zinazotumia teknolojia ya LCD(Liquid Crystal Display).
Kwa kunukuu wamesema"Simu hii inakuja katika wakati ambao smart devices zinatumika sana na haijwahi pata tokea na hatari za simu kudondoka na kuvunjika zikiwa kubwa sana"
Bwana Yoon Bu-hyun makamu raisi wa kampuni hiyo alitangaza wazi mwezi jana kwamba simu hii itazinduliwa katika robo ya mwisho ya mwaka.
Hata hivyo makampuni mengine yanaitolea jicho hiyo teknolojia .Katika mkutano wa Computer Electronics Show uliofanyika mapema mwaka huu Samsung alionesha teknolojia kama hii na kuiita Youm,ambayo itawezesha kutengeneza vioo ambavyo vinakunjika,kuviringisha na hata kupinda.