Showing posts with label ogyoutube. Show all posts
Showing posts with label ogyoutube. Show all posts

Jul 21, 2015

Fahamu Njia Rahisi ya Kupakua (Download) Videos za Youtube Katika PC Yako

Siku si nyingi katika blogu hii tuliandika kuhusu namna ya kupakua videos za Youtube katika smartphone ya Android kwa kutumia app ya OGYoutube,  Unaweza kusoma makala nzima "Njia Rahisi ya Kupakua (Download) Videos za Youtube Ukiwa na App Inayoitwa OGYoutube" HAPA. Kwa upande wa PC, tulielezea kwa kugusia tu. Makala hii itakuelezea namna rahisi ya kupakua videos kwa upande wa PC kwa undani zaidi.

Katika makala iliyopita tuliandika namna ambavyo watumiaji wa PC hupakua videos hizo, tuligusia program maalum kwa kazi hiyo kama vile Internet Download Manager (IDM) na  Free Youtube Downloader kutoka Wondershare. Pia njia nyingine ya kupakua videos hizo ni kuweka extensions kwenye browser ambazo zinafanya kazi hiyo, extensions hizi zinapatikana kwa wingi katika store ya Chrome (Chrome Webstore) kwa ajili ya browser ya Chrome lakini pia hata variants zake zinanufaika na store hiyo, pia kwa wale watumiaji wa Firefox, extensions (add-ons) zinapatikana kupitia Menu kuu ya browser hio.

Hapa ningependa kuelezea njia nyingine ambayo ni rahisi zaidi katika kupakua videos za Youtube, ambayo haihitaji program ya nje kuongeza uwezo wa browser wala haihitaji extension yoyote, njia hii ni kupitia browser yenye uwezo wa ndani (built-in functionality)  wa kupakua videos hizo, na browser ninazozungumzia hapa ni Baidu Browser pamoja na Spark Security Browser. Hizi ni browser mbili ndugu, nikimaanisha kwamba zote zinatengenezwa na kampuni moja, Baidu Global.

Jun 24, 2015

Fahamu Njia Rahisi ya Kupakua (Download) Videos za Youtube Ukiwa na App Inayoitwa OGYoutube

Youtube ni tovuti maarufu sana duniani inayojihusisha na masuala ya kushare videos, ni mahali ambapo unaweza kupata si tu videos za muziki na burudani bali pamoja na videos za kuelimisha na kujifunza masuala mbalimbali. Mara nyingi watumiaji wa Youtube hupenda kupakua (download) videos  zinazowavutia kwa matumizi ya baadaye, lakini Youtube haina uwezo (feature) hii "by default".

Kwa watumiaji wa kompyuta mambo huwa ni rahisi kidogo linapokuja suala la kupakua videos kutoka Youtube. Wengine huweka programu maalum kwa kufanya kazi hiyo, programu kama Internet Download Manager (IDM) kutoka Tonec Inc au Free Youtube Downloader, AllMyTube , Free Video Converter na Video Converter Pro zote kutoka Wondershare hufanya suala la kupakua videos kutoka Youtube kuwa rahisi sana. 

Pia kwa wale wanaotumia browser kama Chrome pamoja na variants zake wanaweza kuweka extensions zenye kufanya kazi hiyo (Youtube/Video Downloaders) ambazo zinapatikana kwa wingi katika store ya Chrome inayojulikana kama Chrome WebStore. Lakini pia ili kufanikisha mchakato wa kupakua videos hasa zilizopo Youtube kuwa rahisi zaidi unaweza kutumia browsers kama Baidu Browser au Spark Security Browser ambazo zimetengenezwa
zikiwa na uwezo wa ndani (built-in capability) wa kupakua video kutoka katika tovuti kama Youtube, hauhitaji extension wala programu yoyote kuwezesha hilo, browser husika ndiyo ina uwezo huo.