Kwa miaka sasa, ushindani mkubwa umekuwepo kati ya Android OS (inayomilikiwa na Google) na iOS (inayomilikiwa na Apple. Operating System ya Android ni tofauti kidogo na iOS, Android ni mradi huru (open source project), inatumika na makampuni mengi yanayotengeneza smartphones (OEMs), makampuni kama Samsung, LG, Sony, HTC, Huawei, Xiaomi na kadhalika yapo katika familia hii. Apple's iOS ni mradi usio na chanzo huru/wazi (closed source project), ni devices za Apple pekee ndizo zinatumia OS hii, kama ilivyo kwa BlackBerry OS.
![]() |
| Apple AppStore, Mpinzani mkubwa wa Android pamoja na Muungano Huru wake uitwao OHA (Open Handset Alliance) |
Kwa mwaka jana, stoo ya apps ya Android OS inayofahamika kama Google Play Store imekua kwa kiasi kikubwa hadi kuipita stoo ya Apple, AppStore. Hii ni faida kubwa kwa Android lakini kuna hasara pia katika familia hii. Watengeneza wa smartphones za Android wanashindana wao kwa wao.
