Showing posts with label google I/O. Show all posts
Showing posts with label google I/O. Show all posts

Jul 18, 2015

Fahamu uzuri wa kutumia app ya Google Photos.

Google I/O ni moja kati ya matukio makubwa kabisa katika ulimwengu wa teknolojia hasa katika upande wa bidhaa za kieletroniki zinazotumiwa na watu (consumer electronics) hususan smartphones, tablets na smartwatches, bila kusahau internet inayounganisha vitu (Internet Of Things). Ni mkutano unaokutanisha si tu developers bali hata wadau na watu wengine ambao ni wafuatiliaji wa teknolojia kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Google hutumia mkutano huu kutambulisha teknolojia, bidhaa pamoja na huduma zake mpya. Mkutano huu hufanyika kila mwaka katikati ya robo ya pili ya mwaka (mid quarter two).

Makala hii inalenga kuelezea moja ya huduma iliyotambulishwa mwaka huu katika mkutano huo uliofanyika Mei 28 na 29 huko San Francisco, CA, USA. 
Google Photos ni huduma kutoka Google inayowezesha kuhifadhi picha pamoja  na videos, pamoja na kwamba huduma hii sio mpya sana lakini kwa mwaka huu imefanyiwa maboresho makubwa kiasi kwamba huduma hii sasa inakuwezesha KUHIFADHI PICHA PAMOJA NA VIDEOS ZAKO ZOTE BILA MALIPO, BILA KIKOMO (FREE & UNLIMITED).

Kila mtu anaweza kutumia huduma hii kwa sababu inapatikana katika sehemu(platforms) tatu, Android, iOS pamoja na Web nikimaanisha kwamba kama mtu hana smartphone au tablet ya Android, pia akiwa hana iPhone au iPad bado anaweza kupata huduma hii kupitia browser ya kompyuta yake bila kuangalia mfumo (OS) anaotumia (Windows/ Mac OSX/ Linux). 

May 15, 2013

Nini kipya kitakuja toka Google I/O mwaka huu.

Leo ndiyo siku ambayo mkutano mkuu wa kampuni ya Google unaowakutanisha developers mbalimbali toka duniani kote unaanza,mpaka sasa hakuna cha uhakika ambacho kimethibitishwa kuwepo ila uvumi wa kuzinduliwa android os mpya iitwayo key lime pie na nexus device nyingine mpya.Habari kamili kaa nasi tutakuwa tunakupa updates kadiri mambo yanavoendelea huko Moscone center,San Fransisco,Marekani.