Siku si nyingi katika blogu hii tuliandika kuhusu namna ya kupakua videos za Youtube katika smartphone ya Android kwa kutumia app ya OGYoutube, Unaweza kusoma makala nzima "Njia Rahisi ya Kupakua (Download) Videos za Youtube Ukiwa na App Inayoitwa OGYoutube" HAPA. Kwa upande wa PC, tulielezea kwa kugusia tu. Makala hii itakuelezea namna rahisi ya kupakua videos kwa upande wa PC kwa undani zaidi.
Katika makala iliyopita tuliandika namna ambavyo watumiaji wa PC hupakua videos hizo, tuligusia program maalum kwa kazi hiyo kama vile Internet Download Manager (IDM) na Free Youtube Downloader kutoka Wondershare. Pia njia nyingine ya kupakua videos hizo ni kuweka extensions kwenye browser ambazo zinafanya kazi hiyo, extensions hizi zinapatikana kwa wingi katika store ya Chrome (Chrome Webstore) kwa ajili ya browser ya Chrome lakini pia hata variants zake zinanufaika na store hiyo, pia kwa wale watumiaji wa Firefox, extensions (add-ons) zinapatikana kupitia Menu kuu ya browser hio.
Hapa ningependa kuelezea njia nyingine ambayo ni rahisi zaidi katika kupakua videos za Youtube, ambayo haihitaji program ya nje kuongeza uwezo wa browser wala haihitaji extension yoyote, njia hii ni kupitia browser yenye uwezo wa ndani (built-in functionality) wa kupakua videos hizo, na browser ninazozungumzia hapa ni Baidu Browser pamoja na Spark Security Browser. Hizi ni browser mbili ndugu, nikimaanisha kwamba zote zinatengenezwa na kampuni moja, Baidu Global.