Showing posts with label clues. Show all posts
Showing posts with label clues. Show all posts

Oct 29, 2014

"Kila iPad ni Tablet" na "Si kila Tablet ni iPad".

Kwa muda mrefu kumekuwa na mkanganyiko katika matumizi ya maneno haya mawili, iPad na Tablet. Hapa kuna mambo mawili ambayo hujitokeza mara kwa mara. Kuna wale ambao huita Tablet yoyote iliyo mbele ya macho yao "iPad" na wengine hudhani kwamba iPad si "Tablet", hawa wote wanakosea. Lakini, kabla ya kwenda mbali sana tujue kwanza maana za haya majina mawili.


TABLET - nI kifaa cha kielectroniki chenye ukubwa wa kioo(display) kuanzia inchi 7 hadi inchi 20(Panasonic washawahi toa tablet ya aina hii). Ina uwezo kama smartphones nyingine, kuna zile zinaweza kuweka sim card na kufanya mawasiliano kama ya simu na zile zisizo support sim card, hizi hutumia wireless internet(Wi-Fi) na zinafahamika kama WiFi only tablets, hutumia WiFi tu kwa mawasiliano, huwezi piga simu wala kutuma sms(no GSM communication). Mfano wa tablets ni kama Nexus 7, iPad mini 2, iPad Air, Kindle Fire HD n.k.

iPad - Ni tablets zinazotengenezwa na kampuni ya Apple. Zipo katika muundo mbalimbali, model zake hutofautiana katika sifa(features) kama

Sep 13, 2014

Baadhi ya mambo unayoweza fanya ili kuepuka kununua smartphone feki.

Watu wengi hujikuta katika wakati mgumu pale wanapohitaji kununua smartphone, haijalishi ni kwa mara ya kwanza au wanapotaka upgrade kutoka smartphone moja kwenda nyingine. Hali hii huja kutokana na kuwa na maswali mengi akilini, Operating System gani inayofaa?, smartphone ipi ina camera bora?, ipi yenye battery inayodumu muda mrefu baada ya kuchaji mara moja tu?, brand ipi ina reputation nzuri katika soko?, hayo ni mambo machache tu, yapo mengi sana. Lakini kuna jambo moja ambalo wengi wetu tulio wanunuzi wa simu hutakiwa kujiuliza, na pengine kushindwa kuzingatia swali hili inaweza leta huzuni na masikitiko makubwa katika manunuzi yetu. "Je! smartphone ninayotaka kununua ni original?". Nitaeleza njia baadhi unazoweza kutumia ili mwisho wa siku katika manunuzi yako jibu la hili liwe "NDIYO" .