Showing posts with label Samsung. Show all posts
Showing posts with label Samsung. Show all posts

Feb 19, 2015

Pengine Samsung Galaxy S6 itabadili kasumba ya Samsung.

Samsung, jina maarufu sana unapoongelea vifaa vya kielectroniki(consumer electronics). Smartphones, televisheni, kompyuta, mashine za kufulia, mitambo ya mawasiliano, mashine zitumikazo hospitali n.k vyote hivi hawa Wakorea kusini hutengeneza. Huwa nafurahishwa vile walivyo na mikakati mizuri katika kutangaza bidhaa zao duniani kote. Na morali hii ndiyo inawapelekea kuwa moja ya kampuni kubwa sana duniani zenye mafanikio. Lakini, pamoja na mafanikio yote haya; dosari huwa hazikosekani. Kuna baadhi ya dosari ambazo Samsung anatakiwa kuziangalia kwa kina ili kuweza kuzirekebisha.

Dec 8, 2013

Samsung anafanyia majaribio baadhi ya simu za kati(midrange smartphones) kama zitaweza tumia Android 4.4 KitKat.

Samsung anafanyia majaribio baadhi ya simu za kiwango cha kati(midrange) kama zinaweza kutumia Android 4.4 KitKat bila shida.Listi ya simu hizo imevuja mtandaoni na imetaja simu zifuatazo.

  • Samsung Galaxy S3 Mini
  • Samsung Galaxy S4 Mini
  • Samsung Galaxy Ace 2
  • Samsung Galaxy Fame
  • Samsung Galaxy Core
  • Samsung Galaxy Ace Advance
Kama unakumbuka hapo mwanzo wakati Android version hii inakaribia kuzinduliwa Google alisema ya kwamba version hii itaweza kufanya kazi katika simu zenye uwezo mdogo kabisa(low end) zenye hadi RAM ya uwezo wa 512MB.
Endapo majaribio ya KitKat yatafanikiwa katika simu hizi basi watumiaji wake wataweza pata official update hapo mwakani baadaye.Hii inatokana na kwamba mpaka simu zote za hali juu(high end) zipate update ndipo midrange zitafuata.

May 23, 2013

LG vs Samsung,hadithi iliyonyuma kuhusu mapambano kati ya hizi kampuni mbili kubwa za kutengeneza vifaa vya kielectroniki.

Ushindani kati ya LG na Samsung unafahamika wazi.Kampuni hizi mbili ambazo ni za Korea ya Kusini ambazo makao makuu yao yapo Seoul yamekuwa katika ushindani kwa zaidi ya miaka 50.Kila mmoja huwa anaangalia mwenzake atafanya nini kipya ili na yeye aje na zaidi ya kile anacvhotaka kuzindua mwenzie.Siri zimeibiwa,tuhuma zilishatokea,mahakamani kesi zishapelekwa kwa kugombea umiliki halali wa baadhi ya uvumbuzi kati ya haya makampuni mawili kila mmoja akitafguta udhaifu wa mwenzie.Wiki chache zilizopita kulikuwa na mashtaka kuhusu nani ambaye ndo ameanzia teknolojia ya OLED(Organic Light Emitting Diode). Hivi karibuni polisi walivamia moja ya ofisi za Samsung ili kuchunguza baada ya LG kudai anafatiliwa uvumbuzi wake na Samsung.Na hata inafikia kiasi kwamba ulinzi uliopo katika makao makuu ya ofisi hii ni mkali zaidi ya ule wa uwanja wa ndege.Mabegi hukaguliwa,kamera zinaachwa nje,kifaa chochote chenye kuhifadhi kumbukumbu(USB Storage) hakiruhusiwi na kamera za usalama zipo kila kona. Haishangazi kwamba kampuni zote hizi mbili zinaongoza kwa kutengeneza vioo(display) zenye ubora wa hali ya juu.Lakini,huwa mara nyingi wanaleta bidhaa zimazofanana,mfano;mwaka huu wote walileta TV ya kwanza ya teknolojia ya OLED yenye mikunjo(curves). Mbali na hayo yote kampuni hizi sio teknolojia tu,ni mfumo wa maisha na watu wengi sana waliojiriwa katika makampuni haya wako radhi kutumia muda wote kufanya kazi katika makampuni haya mpaka muda wa kustaafu utapowafikia.Tofauti na makampuni makubwa ya Ulaya na Marekani haya yanajitoa sana katika kukuza uchumi wa nchi yao,kila mwaka huchukua vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali na kuwaajiri na wengi wao huwa wanaishia kufanya kazi katika makampuni haya mpaka wanapokuja kustaafu.

May 15, 2013

Samsung imesafirisha Samsung galaxy s4 milioni sita,yavunja rekodi yake iliyopita

Hakukuwa na shaka kabisa kwamba Samsung galaxy s4 itakuwa ni simu yenye mafanikio makubwa katika soko la simu,swali lilibaki,je!itaweza kuvunja rekodi iliyoweka nyuma ya simu zake zilizopita kama samsung galaxy s3 na galaxy note 2? Kampuni hii ya Kikorea imeweza kusafirisha zaidi ya simu milioni sita aina ya galaxy s4 ambayo ndo flagship smartphone ya kampuni hii kwa sasa hadi ijumaa iliyopita ikiwa ni wiki mbili toka simu hii iingie sokoni.Lakini mauzo ya juu yalitokea siku nne za mwanzo ambapo ziliuzwa simu zipatazo milioni nne. S4 inaweza kuwa na mwendo ule ule wa kufanya vizuri toka iingie sokoni,watengenezaji hawa wanaweza kufikia malengo yao ya kuuza simu milioni kumi ndani ya mwezi mmoja toka kuzinduliwa kwake.Ukiangalia flagship za nyuma kama samsung galaxy s3 ilichukua siku 21 kufikia mauzo ya simu milioni tatu wakati samsung galaxy s2 ilichukua siku 55,galaxy s ilichukua siku 85 kufikia mauzo ya simu milioni tatu. Pamoja na mchuano mkali Samsung inayopata kutoka kwa simu wenzake za makampuni mengine kama HTC One na Sony Xperia Z ambazo nazo hazina muda mrefu toka kuingia kwake sokoni bado inauza vizuri sana karibu mara kumi ya flagship zake zilizopita kama galaxy s2 na s3.

May 13, 2013

Samsung kuanza kutoa huduma ya internet ya 5G kuanzia mwaka 2020

Mabadiliko katika teknolojia ya mtandao yamekuwa sana kiasi kwamba kila mwaka kunakuwa na mbadiliko makubwa sana na kupiga hatua katika binadamu kuweza kupambana na mazingira yake.
Kutoka katika enzi za kutumia kutumia GPRS lakini sasa teknolojia ya 4G inatumika na kukupa internet ya haraka mno pamoja bado haijafika katika nchi zetu hizi za Afrika.Pamoja na hayo kampuni ya samsung imesema itaanzisha teknolojia nyingine ya internet itayoitwa fifth generation(5G) ambayo itakuwa na kasi ya kuweza kudownload 1gigabyte kwa sekunde ina maana unaweza download movie kwa chini ya sekunde moja,hii ni hatua kubwa ya kurahisisha mawasiliano.