Jun 23, 2015

Njia rahisi kabisa ya kuroot smartphone ya Android OS.

Kipindi cha nyuma nilishawahi kuelezea katika blogu hii maana ya rooting. Katika operating system ya Android, rooting ni mchakato wa kufungua mfumo(system) wa Android ili kuweza kupata uwezo zaidi wa kuitawala smartphone yako. Operating system huwa na makabrasha(files and folders) ambayo huwezi pata uwezo wa kuyafanya chochote mpaka utapofanya mchakato wa rooting.

Unaporoot smartphone ya Android tunasema kwamba umepata "system privileges" ikimaanisha kwamba una vipaumbele vya kuweza kuitawala operating system ya simu yako. Hii itakuwezesha kufuta apps zilizopo katika system, kuzifanya apps unazodownload katika playstore kuwa apps za system(changing application softwares into system softwares), kubadili maandishi(fonts), kuweka operating systems zisizo rasmi(custom roms) na mengineyo mengi.

Kuna njia ambazo hutumika ili kuwezesha rooting kukamilika. Unaweza tumia programu za kompyuta au programu(apps) za Android, inategemea na njia unayochagua kutumia. Kuna baadhi ya njia ambazo hupunguza ugumu wa mchakato huu. Nitaelezea njia moja ambayo kwa sasa ni rahisi sana na inakubali katika smartphone za aina nyingi mno kuanzia Huawei mpaka HTC.

Njia hii hutumia programu(app) ambayo utaidownload na kuinstall katika smartphone yako, app inafahamika kama Towelroot. Kwa kutumia app hii, rooting ni mchakato wa dakika moja tu!. Nitaeleza hatua za mchakato huu. 



1. Katika smartphone yako ya Android ingia katika internet browser uliyonayo na kisha tembelea address hii: http://towelroot.com au unaweza ingia moja kwa moja kupitia hapa. Kisha bonyeza alama ya lambda ili kuweza kudownload file la Towelroot. 

Bonyeza lambda ili kuweza download towelroot.apk
2. Baada ya kukamilisha kudownload towelroot.apk, ingia katika settings za smartphone yako na kisha nenda katika security. Ndani ya security tafuta mahala palipoandikwa "unknown sources", hakikisha sehemu hii ipo activated.

Hutaweza install "towelroot.apk" kama unknown sources ipo deactivated.

3. Baada ya kukamilisha hatua ya pili, rudi katika internet browser yako kisha install "towelroot.apk".

4. Baada ya kufanya installation, fungua app ya towelroot katika menu yako. Baada ya kufunguka, bonyeza palipoandikwa "make it ra1n" .


Hakikisha simu yako ina mtandao(internet) wakati unafanya hatua hii.

5. Kama rooting imekubali katika smartphone, utatokea ujumbe unaoonekana hapo chini katika screenshot. Kama smartphone yako itakataa kuwa rooted kwa hii app itajizima na kujiwasha, hakutakuwa na madhara yoyote.


Kufikia hatua hii, smartphone yako inakuwa rooted.
 6. Baada ya hapo, utahitaji kudownload app kwa ajili ya kupata ruhusa za kuingia katika system ya Android. App hii inaitwa Super User(SuperSU). Utaipata Playstore, ingia Playstore na kisha tafuta "SuperSU" halafu install.

                                           



 7. Baada ya installation, fungua SuperSU na kisha update kwa kuchagua continue, updte kwa kutumia "normal". 

                                           




   8. Baada ya ujumbe unaoonekana hapo chini kukamilika kwa kusema "installation complete". Hapo utakuwa tayari umesharoot smartphone yako ya Android, tayari kuitumia kama Super User. Utahitajika kureboot na baada ya hapo unakuwa umekamilisha mchakato mzima.

                                            

Ili kuangalia kama mchakato wa kuroot umefanikiwa kabisa, unaweza kutumia app ambayo inafanya kazi ya kuangalia root access kwenye simu yako, chagua langu huwa ni hii hapa ambayo inapatikana PlayStore "Root Checker". Lakini zipo nyingi sana playstore, chaguo ni lako.






                

No comments :

Post a Comment