Jan 11, 2015

Jinsi ya kujiunga na internet kiusahihi katika smartphone yako (Android smartphones).

Internet ni muhimu sana katika smartphones. Simu za aina hii zina uwezo mkubwa wa spidi ya internet ukilinganisha na simu za kawaida (feature phones). Nimeandika kidokezi hiki kutokana na kwamba watu wengi hupata usumbufu katika kupata ubora kamili wa internet katika smartphones zao. Unaweza kukuta ya kwamba network ipo vizuri lakini internet ipo slow, hali hii mara nyingi hutokana na kutokuwa na settings zilizo sahihi katika simu yako. Njia nitayoeleza hapa haichagui aina ya mtandao unaotumia, settings hizi zitakubali katika mitandao yote.


KWA SMARTPHONE ZA ANDROID. 


1. Ingia katika menu ya simu yako.



2. Kisha chagua settings.



3.Ingia katika mobile networks.



4. Kisha, ingia sehemu iliyoandikwa access point names.



5. Bonyeza sehemu ya options, kisha chagua "new APN".



6. Itadisplay screen itayokutaka kujaza sehemu(fields) mbalimbali.



7.Katika sehemu ya Name andika neno "internet" na katika APN andika "internet" pia. Baada ya kujaza sehemu hizo mbele,usijaze chochote katika sehemu zilizosalia.




8.Save akaunti kisha activate kwa kubonyeza kitufe cha duara pembeni mwa akaunti hiyo.




9.Hakikisha mobile data imewekewa tick/kuiweka on(utaipata baada ya kufungua mobile network).




10. Hakikisha data roaming haijawekewa tick(hii inapatikana chini ya mobile data.




11. Baada ya hapo sehemu network itatakiwa kuonyesha herufi H au E, ni nadra sana kukuonyesha herufi G.




Hapo unaweza kuanza kutumia internet katika simu yako.

MAELEZO MUHIMU.

H inaashiria HSPA(High Speed Packet Access), HSPA ni muunganiko wa mifumo miwili ya mawasiliano ya kimtandao yaani HSDPA(High Speed Data Packet Access) na HSUPA(High Speed Uplink Packet Acess).  Mara nyingine HSPA hutokea katika alama ya  H+ ikisimama kama Evolved HSPA, boresho la huduma ya HSPA. Aina hii ya mawasiliano ya internet ina uwezo hadi spidi ya 337Mbps katika kupakua data. Mfumo huu ni maboresho ya huduma ya 3G( Third Generation).

E inaashiria EDGE, ikiwa inafahamika kwa jina lingine la 2.75G. Ni maboresho ya mfumo wa mawasiliano wa GPRS(General Packet Radio Service). 


G inaashiria GPRS, ambayo nimetaja kirefu chake hapo juu. Muda mwingine inafahamika kama 2.5G. Kati ya hizi zote yenyewe ndiyo ina uwezo mdogo wa kutuma na kupokea mawasiliano ya kimtandao. Mara nyingi hutumika katika simu za kawaida (feature phones). 



No comments :

Post a Comment