Katika smartphones 210 milioni zilizouzwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu,156 milioni zinatumia android.Huo ni muongezeko wa juu wa asilimia 17.5 ukiangalia kipindi kama hiki kwa mwaka jana.
Research in motion watengenezaji wa BlackBerry ni wa tatu wakiwa wameuza simu zipatazo 6.2 milioni,wakati microsoft ikiwa ikishusha pumzi kwa mauzo ya 6 milioni katika opearting system yake mpya. Samsung anaendelea kuwa namba moja katika watengeneza smartphones na anashikilia asilimia 30% ya mauzo yote,Kampuni ya Korea Kusini imeuza simu 64.7 milioni.Hiyo ni mara mbili ya simu kampuni ya Apple walizouza,wakiwa na mauzo ya asilimia 18.2% na kuuza simu 38.3 milioni.Unaweza kuona makampuni mengine katika chati hapo chini.


No comments :
Post a Comment