Showing posts with label software update chaos. Show all posts
Showing posts with label software update chaos. Show all posts

Dec 31, 2014

Yaliyojiri Mwaka 2014 Katika Teknolojia Ya Smartdevices (2/2).

Televisheni za ubora wa 4K (Ultra-High Definition) 

Siku hizi, watu wengi wanapowaza kununua televisheni mawazo yote huwa katika flatscreen TV. Lakini, kinachofanya TV hizi kuwa ghali si ukubwa wake, ni aina ya teknolojia itumikayo katika hizi TV, kuanzia software yake, display inayotumika na ubora wa vifaa vingine viundavyo TV hiyo. 4K TV ni aina ya runinga yenye uwezo wa kuonyesha ubora wa picha ulio na kiwango cha 4096 (4K) pixels katika resolution ya upana (horizontal resolution), resolution hii kwa jina lingine inafahamika kama Ultra-High Definition (UHD).

Tofauti ya picha kati ya Full-HD na Ultra-HD
4K TV zina uwezo wa kutoa ubora wa picha mara nne zaidi ya Full-HD TV ambazo horizontal resolution yake ni 1080pixels, kuna baadhi ya 4K TVs ambazo zina umbo la kujikunja pia (Curved TVs). TV nyingi za flatscreen zilizo nafuu zina uwezo wa aitha HD katika 720pixels au Full-HD katika 1080pixels. LG na Samsung ni kampuni zilizo maarufu sana na zenye mafanikio makubwa katika teknolojia hii, pia Sony, Philips, Toshiba, Panasonic na Asus hawapo nyuma katika utengenezaji wa TV za teknolojia hii.