Tulio wengi huwa na shauku kubwa sana wakati tunasubiri Operating System(OS) mpya ku update devices zetu, iwe ni tablet au smartphone... shauku ni ile ile. Mategemeo yetu makubwa huwa ni kwamba tunajua tutapata features nyingi mpya, muonekano (User Interface) utaboreshwa na pia baadhi ya matatizo(software bugs) yaliyokuwepo katika version ya OS iliyopita yatapata ufumbuzi. Software update inaweza fanyika kwa njia mbalimbali, kama kutumia programu ya kompyuta(desktop manager) kwa kuunga smartphone/tablet kwenye kompyuta kwa kupitia USB( Universal Serial Bus) na kisha kufanya update process. Njia nyingine haihitaji kutumia kompyuta na pia wala haikuhitaji kuwa na utaalamu wowote wa kiufundi ili kuweza kukamilisha process hii, inafahamika kama OTA(Over The Air) update. Kinachofanyika katika process hii ni kwamba itakuja notification ya kukujulisha kama software mpya inapatikana, utatakiwa kuidownload hiyo software na baada ya hapo utakubali kufanya update na baada ya process hiyo kumalizika utakuwa na software mpya na tayari kuanza kufurahia features mpya. Lakini je! ni mara zote huwa tunafurahia software mpya?