Uchaguzi wa smartphone umekuwa mgumu sana siku hizi, hasa inapofika wakati wa kuchagua ni smartphone ipi ambayo utatumia pesa yako kuinunua. Ugumu huu ni suala la kawaida, hutokana na kwamba aina za smartphones zimekuwa nyingi mno. Watengenezaji waliokuwepo tangu miaka ya nyuma wanazidi kutoa matoleo mapya mara kwa mara, wale wapya nao wanaamka kila siku kuingia katika ushindani wa biashara hii. Afgreenwireless tunakusaidia kukupa listi ya smartphones tatu ambapo kati ya hizi utapata moja inayokufaa kutokana na mahitaji yako. Katika tatu bora hii tumeangalia vitu vikuu kama; uwezo wa battery, uwezo wa processor, ubora wa display, uimara na mengine baadhi. Tumeangalia pia mifumo mbalimbali ya maisha watu wanayoishi, mtu wa ushirika(corporate person) hawezi kuwa na mfumo wa maisha sawa na mwanafunzi wa chuo ambaye anapendelea muziki na sanaa. Watatofautiana vitu vingi katika maisha yao, hata mahitaji yao ya smartphones yatakuwa tofauti. Tumejitahidi kuangalia utofauti kama huu katika kuishi kwa kuangalia mahitaji ya kila mtu katika high end smartphones.
Showing posts with label novemba. Show all posts
Showing posts with label novemba. Show all posts