Inashangaza sana hii kitu,simu ya Nokia Lumia 800 imekutwa ikifanya kazi baada ya kuzama kwenye ziwa kwa miezi mitatu na nusu.
Inaweza kuwa ngumu kuamini jambo hili.Imetokea huko Sweden na kisa hiki kimesimuliwa na Roger Nilsson katika ukurasa wake wa Facebook.Baada ya simu kudumbukia ziwani,ilijificha katikati ya miamba miwili.Baada ya kuokotwa ilikuwa imezungukwa magamba na Algae.Huyu bwana aliisafisha na baada ya kumaliza aliiweka kwenye chaji na simu ikaanza kuingiza chaji.
Anadai kwamba mpaka sasa hamna tatizo lolote katika simu hiyo na inakaa na chaji siku mbili kama kawaida yake.
Kama anachosema ni kweli,basi ni kitu safi sana kwa simu isiyokuwa na specifications za kuzuia maji kuweza kuhimili muda wote huo.Pia,itawapa sifa zaidi kampuni ya Nokia.
Kampuni nyingi kwa sasa wataanza tengeneza simu zao zikiwa na sifa ya kuzuia maji.Lakini itakuwa ni zile za hali ya juu(high end).
Showing posts with label lumia. Show all posts
Showing posts with label lumia. Show all posts
Oct 28, 2013
May 14, 2013
Nokia wazindua simu yao mpya ya nokia lumia 925
Simu hii imezinduliwa leo huko jijini London ambapo imeboreshwa sana ukizingatia na flagship yao iliyokuwepo ambayo ni nokia lumia 920.
Uzinduzi huu umekuja wiki moja baada ya wawekezaji wengi kuponda mikakati ya nokia katika kurudi tena katika uwanja wa kuwa mtengenezaji bora wa simu ambapo nafasi hiyo kwa sasa inagombaniwa na Samsung na Apple.
Simu hii imeonesha maboresho makubwa katika camera,na teknolojia yake ni ya hali ya juu kuliko hata iliyotumika katika camera ya flagship ya samsung,samsung galaxy s4,ambapo camera ya nokia lumia 925 ina uwezo wa kuchukua picha ya mnato na video katika mwanga hafifu mfano katika kumbi za disko.
CEO wa Nokia Stephen Elop amesema uamuzi wa kutumia Microsoft software ambayo inajulikana kama windows phone OS inaaipa nafasi kampuni yake ku compete na kampuni nyingine kama Samsung.
Aina hii itaweka sokoni kuanzia mwezi wa sita Ulaya na China,ikifuatiwa na Marekani na maeneo mengine.
Ina processor ya snapdragon s4 na battery yake 2000mAh hii ni wazi itakuwa ni battery nzuri inayokaa muda lakini hata hivyo imezidiwa na Samsung galaxy s4 yenye 2600mAh.ina 16GB internal memory lakini 32GB version ipo njiani kuja.tutakuletea a full review ya hii simu siku chache zijazo.
