Huwa inatokea, labda umeibiwa au kupoteza simu yako au unataka kubadili simu au labda umeifanyia simu yako system restore iwe ni kwa kukusudia, bahati mbaya au hata kwa kutaka kutibu (resolve) tatizo fulani mpaka ikapelekea kufanya hivyo. Unaweza poteza data nyingi, lakini kikubwa na cha muhimu zaidi ambacho hupotea huwa ni namba za mawasiliano (Contacts).
Hali hii inapotokea huleta huzuni na pia hasira kwa baadhi ya watu na hii yote ni kwa sababu ya hasara iliyotokea. Lakini unaweza hifadhi contacts zako na endapo utazipoteza au chochote kutokea basi utaweza kuzipata kirahisi tena. Nitataja njia chache muhimu unazoweza kuzitumia kama ifuatavyo.