Youtube ni tovuti maarufu sana duniani inayojihusisha na masuala ya kushare videos, ni mahali ambapo unaweza kupata si tu videos za muziki na burudani bali pamoja na videos za kuelimisha na kujifunza masuala mbalimbali. Mara nyingi watumiaji wa Youtube hupenda kupakua (download) videos zinazowavutia kwa matumizi ya baadaye, lakini Youtube haina uwezo (feature) hii "by default".
Kwa watumiaji wa kompyuta mambo huwa ni rahisi kidogo linapokuja suala la kupakua videos kutoka Youtube. Wengine huweka programu maalum kwa kufanya kazi hiyo, programu kama Internet Download Manager (IDM) kutoka Tonec Inc au Free Youtube Downloader, AllMyTube , Free Video Converter na Video Converter Pro zote kutoka Wondershare hufanya suala la kupakua videos kutoka Youtube kuwa rahisi sana.
Pia kwa wale wanaotumia browser kama Chrome pamoja na variants zake wanaweza kuweka extensions zenye kufanya kazi hiyo (Youtube/Video Downloaders) ambazo zinapatikana kwa wingi katika store ya Chrome inayojulikana kama Chrome WebStore. Lakini pia ili kufanikisha mchakato wa kupakua videos hasa zilizopo Youtube kuwa rahisi zaidi unaweza kutumia browsers kama Baidu Browser au Spark Security Browser ambazo zimetengenezwa
zikiwa na uwezo wa ndani (built-in capability) wa kupakua video kutoka katika tovuti kama Youtube, hauhitaji extension wala programu yoyote kuwezesha hilo, browser husika ndiyo ina uwezo huo.
zikiwa na uwezo wa ndani (built-in capability) wa kupakua video kutoka katika tovuti kama Youtube, hauhitaji extension wala programu yoyote kuwezesha hilo, browser husika ndiyo ina uwezo huo.