Ilikuwa mwishoni wa mwaka 2008, nilimuona mtu mmoja akitumia iPhone 3GS, wakati huo ikionekana kama iPhone 6/6 Plus zilivyo sasa. Nilitumia dakika kadhaa katika kuiangalia simu ile lakini kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kusogea nilijiuliza baadhi ya maswali kichwani, "ni kweli hii ndiyo iPhone watu wanayoongelea?"," au pengine hii ni bandia?".... na mengine mengi!
Nadhani maswali hayo yaliyotokana na mimi kuwa na mategemeo makubwa sana kuliko uhalisia wa iPhone 3GS(over anticipation). Vile nilivyosikia watu wanavyoiongelea nilitengeneza picha kubwa sana akilini. Wakati huo, nilikuwa mpenzi mkubwa wa smartphones za Nokia zilizokuwa zinatumia Symbian OS(haipo tena). Symbian OS, iliyokuwa ikitumika katika smartphones za Nokia ilikuwa maarufu sana miaka ya nyuma kabla ya mwaka 2008, ni Android OS ya enzi hizo unaweza kusema! Pengine sikuvutiwa na iPhone ile kwa sababu nilitegemea itakuwa kama smartphone ya Nokia lakini iliyo bora zaidi(more advanced).
Mwaka 2009, mnamo mwezi Juni. Niliona smartphone ya BlackBerry kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Tangu nikiwa mdogo nimekuwa nikipendelea sana vifaa vya kielectroniki hasa simu na saa. Sijawahi kupata furaha ya moyo kama niliyowahi pata siku ile(Eureka moment), ni kama vile mtu yule alinipa simu ile kama zawadi. Nilipatwa na mshangao wa hali ya juu sana, na nikasema hii ndiyo simu inayotoa maana halisi ya smartphone. Kwa muda ule simu hizi zilikuwa gharama sana, ilikuwa ni ngumu kumiliki simu hii kama hutahitaji kutumia pesa nyingi katika manunuzi ya simu, miaka hii simu za kawaida(feature phones) ndizo zilikuwa zikitumika sana.
Leo hii, ukiniuliza" unapendelea smartphones zipi zaidi?", swali hili litakuwa gumu kidogo kujibu! kwa miaka mingi nimekuwa nikitumia smartphones zinazotumia Android OS, kitu kimoja kinachonivutia katika uwanja huu ni UHURU!, hili ni jambo kubwa linalonifanya kuvutiwa sana na Android OS. "Kwa nini BlackBerry haitanitoka moyoni mwangu?".... Ni rafiki na mshirika mzuri sana katika kazi zangu, na ndiyo maana inakuwa ngumu kutoa jibu la haraka haraka smartphone ipi ni zaidi. Kila mmoja katika hawa wawili ana faida zake na hasara zake katika maisha yangu ya kuzitumia platform hizi mbili. Windows Phone OS ni nzuri lakini inachukua muda mfupi sana kuchoka muonekano wake(UI)......iOS! Pengine ndiyo platform yenye nguvu kuliko zote, kwangu mimi hii ni jela, simaanishi iOS si nzuri, hapana! Ni OS bora kabisa lakini si kwa mtu kama mimi..... Kwa kusema!
Inahitaji mapenzi ya dhati kabisa kutumia iOS, ni sawa katika BlackBerry pia. Kuna watu mpaka leo hawataki hata kuzishika simu hizi. Lakini pamoja na mapenzi/ushabiki na vyovyote vile utavyopenda kuita, uchaguzi wa smartphone na hasa pale unapolipa suala la OS kipaumbele, inakubidi kulifahamu haswa chaguo lako. Nimekutana na watu wengi wanaojuta kununua smartphones fulani. " Sikujua kama huwezi kurusha picha katika iPhone kwa kutumia Bluetooth!", "Kumbe BlackBerry hazina application rasmi ya Instagram?", " Windows Phone hazina app ya Google Plus!", sentensi hizi za malalamiko,majuto, huzuni na mshangao nimezisikia mara kadhaa.
Pamoja na kwamba BlackBerry ni kampuni ambayo kwa sasa ina soko finyu sana la smartphones zake, BlackBerry World(store yake ya apps) ina namba ndogo sana ya apps na nyingi zilizopo ni za kulipia, smartphones zake zina mvuto mdogo ukilinganisha na smartphones za makampuni kama Apple na HTC, ndiyo kampuni pekee yenye smartphones zinazotumia OS mbili tofauti(zile zinatumia BlackBerry OS 7.1 na matoleo ya nyuma na zile zinatumia BlackBerry 10 OS), inahangaika katika kurudisha heshima yake iliyokuwa nayo zamani na mambo mengine lukuki. Bado kuna sifa kubwa sana katika smartphones hizi ambayo makampuni mengine yameshindwa kuifikia, ni smartphone zilizotengenezwa(tailored) kwa kukidhi mahitaji ya kazi, hasa za ofisini(corporate purposes). Siku hizi, unapotumia BlackBerry mbele ya watu, unajiweka katika hali ya kuulizwa maswali mengi sana, "Ni aina gani ya smartphone unayotumia?", " Bado watu wanazitumia mpaka leo?", "Zina muonekano gani?", ni mlolongo mrefu sana wa maswali utayoulizwa kila mahala utapokwenda.
![]() |
BlackBerry Z10. |
Katika BlackBerry, nitaongelea kwa upande wa BlackBerry 10 OS ambayo ni ya kisasa zaidi(latest). Uwezo wa kuzip files, kuextract files na kuweza kusoma pdf files huja katika OS yenyewe(pre-installed), hutahitaji kudownload third-party app kwa ajili ya kazi hizi, tofauti na ilivyo katika smartphones nyingi za Android. Third party apps nyingi zinazopatikana katika Google PlayStore mfano za kuextract na kuzip files huwa zinashindwa kamilisha kazi hasa wakati wa kuzip files nyingi sana kwa wakati mmoja.
Katika Android OS ili kuweza pokea barua pepe hapohapo(instantly), kufanya instant sychronisation ya namba za simu unazoongeza katika phonebook yako, ku-update appointments katika calendar yako na mengineyo inakubidi feature inayoitwa "auto sync(automatic synchronisation)" iwe on muda wote. Unapoiweka off feature hii ambayo inapatikana katika settings za smartphone husika hutaweza pokea update ya vyote nilivyotaja hapo mapema. Katika hali ya kawaida, watu wengi huweka feature hii off kuepuka charge kuisha haraka kwa sababu hutumia nishati kubwa sana, hufanya simu muda wote kuwa katika miamala ya kutuma na kupokea taarifa kutoka katika server, ili kuweza kupata barua pepe kwa mfano, itakubidi kufanya synchronisation mwenyewe(manually) kwa kurefresh kila akaunti iliyopo katika smartphone yako. Katika BlackBerry 10 OS, unaweza weka off feature zote ambazo zinapelekea charge kutumika sana lakini barua pepe zitaingia mara moja zinapotumwa na wewe utaweza jibu hapohapo.
Ukiangalia OS za Android, Windows Phone na iOS zina notification panels(sehemu inayoonyesha sms, simu na taarifa nyingine zinazoingia katika simu yako) ambazo zinafanana kwa hali moja au nyingine. Pamoja muonekano(UI) upo tofauti kulingana na OS husika lakini ufanyaji kazi wa kimsingi upo katika kufanana.
![]() |
Notifications zako zote zinakaa mahala pamoja. |
BlackBerry Hub, notification panel katika BlackBerry 10 OS ambayo haijawahi kutokea katika OS nyingine yoyote ile kabla. Ipo tofauti sana ukizilinganisha na nyinginezo hasa ya Android. Katika Android kwa mfano, hakuna uwezo wa kukuwezesha kujua kwa urahisi mlolongo mzima wa miamala katika smartphone yako, hakuna sehemu itayojumuisha simu ulizopiga au kupigiwa, sms za kawaida ulizotuma au kupokea, notification za Facebook,Twitter na nyinginezo katika mahala pamoja. Inakubidi upitie katika kila app kwa upekee ili kufahamu yote haya. Kwa upande wa BlackBerry 10 OS, BlackBerry Hub inawezesha haya yote. Notification zote zinaonekana katika sehemu moja tu, iwe ni barua pepe, simu unazopiga au kupigiwa, tweets, notification za Facebook na nyinginezo. Inakuwezesha kujua kwa urahisi sana ni jinsi gani umewasiliana kwa kutumia simu yako kwa siku nzima... Pengine hata wiki moja iliyopita!. Si hilo tu, unaweza ukafanya mawasiliano yako yote ndani ya BlackBerry Hub bila kwenda katika app husika. Mfano, unaweza kutuma na kupokea sms za Whatsapp ukiwa ndani ya BlackBerry Hub bila kwenda katika app ya Whatsapp kupitia menu ya simu. Kitu ambacho hakipatikani katika OS nyingine.
Katika kazi! BlackBerry ni msaidizi bora sana. Pamoja na kwamba Android OS ni pana sana kutokana na ilivyosheheni features. Nitabaki kuipenda BlackBerry siku zote.......
No comments :
Post a Comment